Hati mpya kupatikana kwenye tovuti zikiwemo: Kanuni za Ligi na Usajili - 2025, Kanuni za Maadili, Kanuni za Uchaguzi, Kanuni za Fedha na Utawala (Machi 2025) na Katiba ya hivi karibuni [Toleo la 2023]
2min
Tumefanya hati muhimu zipatikane katika tovuti yetu, zikiwemo Kanuni za Maadili, Kanuni za Uchaguzi, Kanuni za Fedha na Utawala (Machi 2025), Mwongozo wa Uhusiano wa Kimataifa, Kanuni za Ligi na Usajili [2025] na Katiba ya hivi karibuni [Toleo la 2023].
Bofya hapa ili kuona na kupakua rasilimali hizi muhimu.
TVF imetoa matokeo ya uchunguzi wa sifa za wagombea wa uongozi ambapo baadhi wamepitishwa na wengine wamekatwa. Kamati imetoa utaratibu wa pingamizi na rufaa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.
TVF imetangaza uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 21 Desemba 2025 jijini Dodoma. Fomu zinapatikana kuanzia tarehe 10 Novemba hadi 24 Novemba 2025 kupitia tovuti ya TVF. Wadau wote wa mpira wa wavu wanahimizwa kushiriki kwa kuchukua na kurejesha fomu kwa wakati.
Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania – TVF, linawataarifu wadau wote kuwa dirisha la usajili kwa Vituo na Shule za kulelea Watoto, Taasisi binafsi, Makocha na Waamuzi limefunguliwa kuanzia leo tarehe 2/2/2024 hadi tarehe 16/2/2024.