Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) linawatangazia wanachama na wadau wote wa mpira wa wavu kuhusu uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 21 Desemba 2025 jijini Dodoma. Nafasi mbalimbali zimetangazwa.
4 min
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) inatangaza rasmi kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa TVF utakaofanyika tarehe 21 Desemba 2025, jijini Dodoma.
Nafasi zinazogombewa ni kama ifuatavyo:
- Rais: Nafasi 1
- Makamu wa Rais: Nafasi 1
- Wajumbe wa Bodi (Wanaume): Nafasi 2
- Wajumbe wa Bodi (Wanawake): Nafasi 2
Gharama za Kuchukua Fomu:
- Rais na Makamu wa Rais: TZS 1,000,000
- Wajumbe wa Bodi: TZS 500,000
Fomu:
Fomu na hati nyingine zinapatikana katika link zifuatazo; bonyeza ili kudownload.
👉🏽 Katiba ya TVF [Toleo la 2023]
👉🏽 TVF Electro Regulations 2025
Mwisho wa kurejesha fomu ni Jumatatu, tarehe 24 Novemba 2025 saa 10:00 jioni. Fomu zirejeshwe kupitia barua pepe: uchaguzi@tvf.or.tz
Taarifa za Malipo:
Malipo ya fomu yafanywe kupitia akaunti ifuatayo:
Jina la Akaunti: Tanzania Volleyball Association
Benki: NMB
Namba ya Akaunti: 24510025069
Wakati wa kurejesha fomu, hakikisha umeambatanisha risiti ya malipo (Pay in Slip) kuthibitisha ulipaji wako.
TVF imetoa matokeo ya uchunguzi wa sifa za wagombea wa uongozi ambapo baadhi wamepitishwa na wengine wamekatwa. Kamati imetoa utaratibu wa pingamizi na rufaa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.
Hati mpya kupatikana kwenye tovuti zikiwemo: Kanuni za Ligi na Usajili [2025], Kanuni za Maadili, Kanuni za Uchaguzi, Kanuni za Fedha na Utawala (Machi 2025) na Katiba ya hivi karibuni [Toleo la 2023]
Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania – TVF, linawataarifu wadau wote kuwa dirisha la usajili kwa Vituo na Shule za kulelea Watoto, Taasisi binafsi, Makocha na Waamuzi limefunguliwa kuanzia leo tarehe 2/2/2024 hadi tarehe 16/2/2024.